MADHARA YA KUWEPO SARAFU AINA MOJA AFRIKA MASHARIKI.
Vikao vinavyojadili kuungana kwa Afrika Mashariki vimepiga hatua sasa. Aidha kuna bunge sasa na Idara ya sheria ambazo ni mtikati ili mradi huu kuimarika. Marais vilevile wameanza kwa njia fulani kupokezana uenyekiti kwa zamu. Juzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete amempokeza Mwai Kibaki Uenyekiti kwa kipindi kinachofuatia.
Aidha ili kuwe muungano imara lazima kuwepo aina moja ya sarafu inayotumika kote Afrika Mashariki. Ina maana kwamba hatutahitaji tena mashilingi ya Kenya, Uganda, Tanzania Rwanda na Burundi iwapo maombi yao ya kujiunga na muungano huu yatapitishwa. Ni kawaida kwamba mataifa yanapoungana wanazua sarafu sawia. Haya yametendeka bara Ulaya. Zaidi ya mataifa 15 yaliyo katika muungano wa European Union yamesahau sarafu zao za awali na kubugia hii iitwayo Euro. Inatarajiwa ni muda mfupi tu na Kronar za Uswidi na Norway hazitakuwapo tena sawa na sarafu za mataifa mengine katika muungano huu.
Nguvu za sarafu inayozaliwa huimarika maradufu tofauti na sarafu za mataifa pweke za awali. Ninachomaanisha ni kwamba iwapo dola 1 ya kimarekani ilibadilishwa kwa shilingi 70 za Kenya kabla ya kuungana basi huenda dola moja ikanunuliwa kwa shilingi 10 za sarafu itakayozaliwa baada ya kuungana. Iwapo dola moja ilinunuliwa kwa shilingi 1800 za Tanzania basi itanunuliwa kwa shilingi 10 za sarafu mpya.
Athari ya kwanza ya kuwepo na sarafu iliyo na nguvu kupita kiasi ni kwamba raia wa mataifa mbalimbali watalalamika kwamba gharama ya maisha imepanda japo kwa njia tofauti. Watakaoathiriwa zaidi ni raia wa taifa ambalo lilikuwa na sarafu dhaifu kiasi ikilinganishwa na dola. Hivi ndivyo raia wa Uswidi, Norway, na Ujerumani wanalalamika leo. Wanadai gharama ya maisha imepanda kutokana na kuwepo kwa Euro. Hebu angali hali hii, kabla ya muungano wa E.U. sarafu ya Uswidi ilinunuliwa kwa shilingi 9 za Kenya; hivi sasa Euro inanunuliwa kwa shilingi 87 za Kenya. Hali kama hii itakuwepo mataifa ya Afrika Mashariki yatakapoungana. Dola moja nchini Uganda inanunuliwa kwa zaidi ya shilingi 2000 za Uganda, nchini Tanzania ni zaidi ya shilingi 1500 za Tanzania kisha nchini Kenya ni shilingi 70 za Kenya. Tutakapokuwa na sarafu moja raia wa Uganda watalalamika zaidi ya wenzao kwamba gharama ya maisha imepanda huku raia wa Kenya wakillamika kwa kiasi kidogo tu maanake nguvu za sarafu zaliwa zitapanda kwa kiasi kidogo tu.
Madhara ya pili ni kwamba iwapo haitawekwa sheria ya kulinda uwekezaji, raia wengi wa Kenya wataingia Tanzania na Uganda kwa njia ya kununua ardhi na kuwekeza. Hii ni kwa sababu Wakenya watakuwa na fedha nyingi wakilinganishwa na wenzao Watanzania na Waganda. Sababu ya kuwa na fedha nyingi itatokana na wao kutumia kiasi kidogo cha shilingi za Kenya kununua sarafu mpya. Kwa mfano huenda Wakenya wakabadili sarafu mpya kwa shilingi 5 za Kenya, Watanzania shilingi 20 za Tanzania na Waganda shilingi 50 za Uganda. Hata hivyo iwapo wasomi Watanzania na Waganda wataruhusiwa kuingia katika soko la Kenya pasipo vikwazo basi hali itakuwa imesawazishwa.
2 Comments »
Leave a Reply
-
Recent
- MAREKANI INAVYOFADHILI VITA BARANI AFRIKA.
- MISHAHARA YA WABUNGE KENYA: WIZI! WIZI! WIZI!
- SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI.
- UBAKAJI: NJOKI NDUNG’U ANAFICHA HABARI FULANI.
- MADHARA YA KUWEPO SARAFU AINA MOJA AFRIKA MASHARIKI.
- KUNA HATARI YA KALONZO MUSYOKA KUWA RAIS?
- NAMNA YA KUPIMA UBORA WA MAISHA.
- KIFO NI NINI?
- KITOTO CHA MAREKANI KINASAFIRI ULIMWENGUNI ZAIDI YA MHADHIRI CHUONI AFRIKA.
- KUTOJUMULISHA MIKOPO YA WAFADHILI: HEKO SERIKALI
- MBONA MAREKANI NA UINGEREZA ZINAINGIA TANZANIA BILA BREKI?
- KAMUSI YA ISIBATI
-
Links
-
Archives
- May 2006 (2)
- April 2006 (14)
- March 2006 (12)
-
Categories
-
RSS
Entries RSS
Comments RSS
Ni uchambuzi mzuri. Lakini kwa sasa, dola moja ya Kimarekani inanunuliwa kwa shilingi za Tanzania kati ya 1250/- na 1260/- na shilingi ya Uganda inanunua dola moja ya Marekani kwa kati ya 1685/- na 1692/- kwa Julai 13, 2007.
Ni uchambuzi mzuri. Lakini kwa sasa, dola moja ya Kimarekani inanunuliwa kwa shilingi za Tanzania kati ya 1250/- na 1260/- na shilingi ya Uganda inanunua dola moja ya Marekani kwa kati ya 1685/- na 1692/- kwa Julai 13, 2007.Na pia Norway si mwanachama wa Muungano wa Ulaya