kwangila

Just another WordPress.com weblog

NAMNA YA KUPIMA UBORA WA MAISHA.

Kunavyo vigezo mbambali wanavyotumia watu kupima ubora wa maishayao. Baadhi yetu tutatumia mali tuliyonayo kama vile majumba, biashara na mafedha tuliyoweka benki. Wengine tutapima maisha kwa vyeo tulivyo navyo katika jamii kwa mfano mwanasiasa atajiona kuwa bora zaidi kuliko raia wa kawaida. Kisha kunao watatumia elimu kudai kwamba maisha yao ni bora. Hivyo basi profesa atajiona kuwa miongoni mwa watu wachache walio na maisha bora . Wengine watatumia vigezo vya familia. Hivyo basi dume lililo na mke mrembo au watoto watiifu na werevu shuleni atajiona kuwa bora zaidi. Lakini swali linabakia kuwa kilele cha maisha bora ni nini? Ni mapesa, ni vyeo, ni familia, elimu?

         Kwa mujibu wa wanasaikolojia, ubora wa maisha ni jumla ya vipengele vingi. Kipengele kimoja ni jiwe lisiloweza kuijika chungu. Hii ndiyo sababu tajiri aso mke hatakuwa na maisha bora. Hii ndiyo sababu Profesa asokuwa na mali hatajihesabu kuwa na maisha bora. Mwanasiasa asiyekuwa na elimu atajiona duni katika bunge na mara nyingi atanyamaza kimya mijadala inapoendelea bungeni.

         Ukitaka kujua watu uliodhani wana maisha bora sivyo ilivyo, nenda nchini Kenya umpate bwana wa umri wa zaidi ya miaka 50 aliyeamua kujiunga na shule ya msingi licha kwamba anamali. Njoo Marekani ukutane na wanawake wenye dola lakini wameishia katika vyumba vya washauri maanake hawana wenzi katika maisha yao. Rudi nchini Kenya tena ukutane na rais Kibaki ambaye licha ya kudhani kwamba maisha bora ni kuwa rais, ametajwa na upinzani kuwa mhusika katika ufisadi serikalini. Kisha baada ya safari hizo tatu ujilize kwa nini wasomi wengi siku hizi wanajitia kitanzi? Wengi wanajitosa majini, wengine wanajitia mikanda shingoni huku wengine wakibugia sumu.  

            Kwangu mie nikidhani wa ubora maisha hupimwa kwa kiwango cha furaha alicho nacho mtu. Si lazima uwe na mali nyingi kupindukia wala elimu ya hali ya juu ili uwe na furaha. Vilevile furaha hailetwi na cheo alicho nacho mtu katika jamii wala kuwa na familia pekee.

Advertisements

April 15, 2006 - Posted by | Uncategorized

3 Comments »

 1. Siku hizi watu wengi wanauliza kama wazungu”are you happy?” au utawasikia “I am happily married” Mie nikidhani furaha ni kitu cha kupita kama vile ilivyo huzuni. Ukitaka kumpata mtu mwenye raha na furaha wakati wote huyo hatuwezi kumpata.
  Nafikiri, kuwa na amani na kuridhika ndiyo jambo la kutafutwa. Basi katika maisha ya leo ambayo mali ndio kipimo cha utu si rahisi kupata muwafaka kati ya mali na furaha. Utu na mahusiano mema na walio karibu na mtu ndio humpa mtu amani – wala siyo kisomo au mali, kwani yakishapita yote bado tu binaadamu tunaoishi katika jamii, hivyo mahusiano mema pekee ndio yatakayoleta amani nafsini – hivyo furaha ya muda mrefu.

  Comment by mwandani | April 18, 2006 | Reply

 2. ukitaka kujua maisha yamejengwaje bwana kwingila soma mhubiri sulemani alikuwa na kila kitu bado hakuwa na furaha lakini kabla maisha yake yalibeba upole na unyenyekevu ndio maana wazungu wanasema power corrupt kwa sababu mtu kabla ya kuwa na nguvu ni muumini mzuri lakini akishapata mtafute
  bado sijafungua blog lakini nipo mbioni nahitaji suport yenu

  Comment by minja | October 18, 2006 | Reply

 3. tafadhali majamaa..hebu, ukiwa unataka ku advertise chochote kile, julisha watu bure 100%, kwa mtandao, http://www.mapeni.com

  ahsante, julisheni wengine wapate advertisement ya bure pia.

  Comment by nicholas | January 15, 2010 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: