kwangila

Just another WordPress.com weblog

MBONA MAREKANI NA UINGEREZA ZINAINGIA TANZANIA BILA BREKI?

Tanzania juzi wamesamehewa madeni. Huzuni iliyoje? Ninaposema huzuni nikidhani Boniphace Makene ananielewa. G8 (mataifa yenye utajiri mkubwa duniani) yalikutana na kuisamehe nchi ya Tanzania madeni. Madeni haya yalikuwa mengi kutoka IMF na World Bank. Si madeni kutoka nchi mahususi kama vile Marekani au Uingereza.

IMF na World Bank ni mali ya mataifa ya ulimwengu. Mataifa mengi yamewekeza katika taasisi hizi mbili. Hivyo basi kusamehewa kwa madeni kuna maana kwamba ni ruzuku kutoka mataifa ya kilimwengu. Hivyo basi hasara kwa washikadau pweke si kubwa mno. Lakini swali Wabongo wanastahili kujiuliza mbona baada ya ruzuku hii Marekani na Uingereza wameingia bila breki kuikopesha Bongo?

Marekani na Uingereza wanajua kwamba wanapochukua nafasi hii kwanza, kabla ya mataifa mengine, basi Tanzania itaanza kulipia mikopo yao kwanza kabla ya kuanza kulipia mikopo mingine kutoka mataifa mengine.

Pili Marekani na Uingereza wametumia fedha nyingi sana katika vita vya Iraq. Hivyo basi wanawekeza mali yao kwa lazima katika mataifa maskini ili izae faida kwa haraka kufidia hasara waliyopata katika vita hivi vya Iraq. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa kwamba faida watakayodai kutokana na mikopo waliyoipa bongo itapanda.

Mataifa haya mawili yamezistadi hotuba za Kikwete na kujua udhaifu wake. Wamejua namna ya kumfurahisha ni kumpa mikopo kwa taifa lake ili kupambana na ufisadi. Kumbuka kuwekeza katika kupambana na ufisadi hakuleti faida ikilinganishwa na iwapo mikopo ile ingewekezwa katika viwanda. Hii ni njia moja ya kuongeza muda wa kulipa mikopo ile. Wanalazimisha mataifa pokezi kutumia mikopo katika miradi isiyoleta faida. Muda unapoongezeka basi ina maana faida kwao kwa kila mkopo.

Nikidhani mataifa haya yanaogopa Marais waliosomea uchumi na siasa maanake wanajua sera zao zitahakikiwa kabla ya misaada yao kukubaliwa. Wabongo mwasemaje?

Advertisements

April 9, 2006 - Posted by | Uncategorized

4 Comments »

 1. Ahsante kwa kunitembelea.

  Comment by mdadisimkenya | April 10, 2006 | Reply

 2. Kyeu, mimi haya mambo nilishayakimbia kabisa, misaada na mikopo ina madhara makubwa kuliko faida yake. Misaada na mikopo kama ulivyosema hapo inalenga maeneo ambayo hayana faida ya haraka kwa umma badala ya kuongeza vita vya kupambana sisi kwa sisi. Tuna kazi ya kutazama hali hizi na kuzikemea au jamii ijiingize kutambua kabla mikopo haijachukuliwa ili kubaini udhaifu wake.

  Comment by boniphace makene | May 6, 2006 | Reply

 3. Haya yote tunayokumbana nayo ni matokeo ambayo watanzania wengi wanayandaa wenyewe katika shughuli zao za kila siku.Kwa mfano, jambo hili la ufisadi halitaisha kwa kupata misaada au kwa kuwaomba watu walioko nje waje watusaidie bali litaisha kwa sisi wenyewe kukamatana mashati kwa namna yoyote ile, kwa ni baadhi yetu wameshasema kama noma na iwe noma au vipi washkaji. Sasa tukumbuke wabongo kila tunalofanya sasa wenzetu wazungu wanaliogopa na wanalichukulia hatua za kujilinda wao mapema zaidi hata ya sisi tunavyotaka kulitekeleza, wakija na vigezo kwamba wanataka kutusaidia na sisi tunataka kuiga mfano wao eti kwa vile wameendelea. Watanzania, nawaombeni sana, mimi huwa nasema, ukitaka kujikwamua katika matatizo, yachukie kwanza ndio utaachana nayo, sasa kuna wengi wetu wanafurahia kupewa misaada, na hii inatokana na kwamba tumesha jihalalishia umaaskini. Kwani katika mikataba ya kimataifa, nchi iliyo masikini inabidi kusaidiwa na zile zilizo matajiri. Ukichunguza kwa undani misaada tunayopewa ni nguvu zetu wenyewe. wanakupa msaada na masharti kuwa unatakiwa ulime, tena wanakupangia na zao la kulima na mbegu wanakuletea tani kwa tani, baada ya kulima si utavuna, ukishavuna tu utasikia bei katika soko la dunia katika zao hilohilo mliloipua ninyi zimeshuka, Sasa waTZ wenzangu niwaambie sio kwamba zimeshuka ni kwamba wanataka waayachukuwe sawa na bure.
  WaTZ sasa tunaelekea katika hali ya juu zaidi ya ukoloni, yaani tunachunwa bila kulazimishwa, hivi nyi hamlioni hilo?? sasa basi swala linakuja tufanyeje. mkikataa kuyauza mazao yenu basi mle wenyewe. wewe mtanzania jiulize kipi bora. Upokee msaada ambao umeufanyia kazi mwenyewe au ujisaidie mwenyewe? maendeleo ya kweli hayatoki nje ya pale ulipo. WaTZ tunauliza njia ya kwenda ktk maendeleo wakati tumekanyaga juu yake.

  Kitu kingine kinachonishangaza mimi ni huku kujifaragua kwa viongozi wetu hasa wale waliokuwa madarakani katika serikali zilizopita,utajifanyaje sasahivi umebadilika unajua la kufanya wakati takribani miaka mingi hukufanya unayotaka kufanya sasahivi, je huoni kuwa umepoteza muda wa watanzania bure? ukiwauliza huwa wanasema hivi(naomba niseme kwa kiingereza) “I WAS NOT IN A POSITION TO SAY” Sawa tunafahamu maneno yalikuwa ni yako na yako kinywani mwako, lakini TANZANIA si yetu hii hii moja iweje wewe uwaache watanzania wenzako wapotee kwa miaka mitano au kumi eti unasubiri ukija kuingia wewe ndo utarekebisha, WASIPOKUPA JE? utakaa nayo ndani. SASA JAMANI WATANZANIA, UU SIO IJUNGA KWELI? NAOMBENI TUUACHE MARAMOJA.
  AKHSANTENI SANA

  Comment by MUGUSHA LEOPOLD | July 11, 2006 | Reply

 4. Nilitaka kusahau Watanzania wenzangu, naombeni mnisaidie kwa hili;
  HIVI KUNA MTU ALISHAKAA AKAJIULIZA SOKO LA DUNIA LIKO WAPI? HUKO AMBAPO SIJUI NAFAKA ZINAKUWAGA NYINGI KIASI CHA KUSHUKA BEI KWA NAFAKA ZA SEHEMU FULANI.

  MIMI NINAVYOFAMAMU, SOKO LA DUNIA NI VICHWA VYA WATU WACHACHE WALIOSHIKILIA DUNIA AMBAO TUSIPOWATHIBITI SASA WANAWEZA HATA WAKAISIMAMISHA ISIZUNGUKE KWAO KUKABAKI MCHANA NA KWETU KUKAWA USIKU MILELE.

  Comment by MUGUSHA LEOPOLD | July 11, 2006 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: