kwangila

Just another WordPress.com weblog

KAMUSI YA ISIBATI

Kama mwalimu wa Isibati nimeanza kutayarisha kijikamusi cha Isibati kwa Kiswahili. Nawaalika wataalamu wa Isibati kuihakiki kijikamusi hiki kadri ya uwezo wao. Nimelazimika kuswahilisha msamiati mwingi maanake hivi sasa sina suruali, inanibidi niazime kutoka kwa jirani kabla ya kupata suruali yangu. Ongeza visawe, punguza au zua mjadala utakaofanikisha mradi huu. Kamusi yenyewe i hapa chini.

KAMUSI YA ISIBATI 

Kiselelisheni/Accerelation.

Namna ambavyo velositi hubadilika na wakati.

 

Ekwishoni Ajebura (Algebraic Equation)

Ni ekwishoni yenye umbo la f(x)=0: pale ambapo f ni Polinomio

 

Otitudi(Altitude)

Otitudi ya traiango ABC ni mstari kutoka vatekisi moja ya traiango ile hadi kwenye k.m Vatekisi A. Mstari huu hugawa
Mstari BC wa traiango ile kwa vipande sawa.

 

Ango(angle)

Mistari au pleni mbili zinapokutana kinachoundwa ni ango.

 

Wastani wa Kiarithimetiki/Avareji(Arithmetic Mean/Average)

Ni mgao wa hesabu ya vitu na idadi yake. K.m. iwapo thamana ya vitu ni ‘m’ na  idadi ya vitu vile ni ‘n’ basi Avareji yake ni m/n.

 

Besi.(Base)

Katika ekipreshoni xⁿ , X ni besi huku y ikiwa ekisoponenti.

 

Namba bainari.(Binary number)

Ni nambari yenye besi namba 2

 

Baisekiti.(Bisect)

Ni kugawanya mara mbili. Vipande view sawa.

 

Biti.(Bit)

Hii ni dijiti bainari

 

Baiti.(Byte)

Ni kiwango cha memori kinachohitajika kuwakilisha karakita moja katika tarakilishi. Idadi yake huwa ni bit inane.

 

Ango Kati. (Central Angle)

Ni ango iliyo kati ya rediasi mbili.

 

Khodi.(Chord)

Ni mstari unaounganisha pande mbili za kavu Fulani.

 

Duara/ Sako. (Circle)

Umbo mzunguko ambalo sehemu zake huwa na urefu sawa kutoka sehemu iliyo kati.

 

Koni Duara. (Circular cone)

Ni koni ambayo tako

lake
ni duara.

Sakamusenta. (Cicurmcenter)

Sakamusenta ya traiango ni sehemu kati ya duara ilyochorwa ndani ya traiango ile.

 

Koefishienti.(Coefficient)

Ni konsonanti ambayo huzidishwa na kibadiliki Fulani katika polinomio.K.m. katika Polinomio X²+3X+7, Koefishienti ni 1, 3 na 7.

 

Ango Komplimentari. (Complimentary angles)

Hizi ni ango ambazo jumla yazo ni 90°

 

Nambari tata. (Complimentary angles).

Ni jumla ya nambari halisi nay a kufikirika. Km 3+4i pale ambapo i=√-1.

 

Konikevu. (Concave)

Umbo lililopindika ndani.

 

Maumbo kongurenti.(Congruent figures)

Ni maumbo ya kijometriki yanayolingana kwa ukubwa na umbo.

 

Kubu.(Cube).

Ni umbo yambisi lenye mistari sita inayolingana kwa urefu na kufungamana.

 

Ekwishoni kubiki.(Cubic equation)

Ni ekwishoni polinomio ya digrii 3

 

Dekagoni.(Decagon)

Ni polinomio yenye pande 10.

 

Nambari nukta. (Decimal number)

Ni nambari iliyoandikwa kwa kutumia besi 10.

 

Digrii.(Degree)

Digrii ya umbo lolote lile lenye vibadiliki ni ekisiponenti ya variabo/kibadiliki kile. K.m digrii ya 7X³ ni 3.

 

Dinomineta.(Denominator)

Atika nambari mgao x/y, x huitwa numereta nayo y ikatwa dinomineta.

 

Dayagono.(Diagonal)

Katika poligoni mstari unaounganisha vatekisi moja na nyingine isokuwa karibu huitwa dayagono.

 

Dayamita/Diameter

Katika umbo-duara, dayamita ni mstari unaopitia katikati mwa duara ile.

 

Dijiti/Digit

Ni nambari zifuatazo: 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9

 

Divaisa/Divisor

Katika nambari mgao a/b, a huitwa dividenti ilihali b ikawa divaisa.

 

Dodekagoni/Dodecagon

Hii ni Poligoni yenye pande 12.

 

Dodekahiduroni/Dodecahedron

Ni umbo yabisi/solid yenye nyuso 12.

 

Domeni/Domain

Domeni ya fankishoni f(x) ni mfululizo wa thamana ambazo x imepewa.

 

Elipsi/Ellipse

Ni umbo pleni ambalo ekwishoni yake ni x²/a²+y²/b²=1

 

Elipusoidi/Ellipsoid.

Ni umbo yambisi ambalo ekwishoni yake ni x²/a²+y²/b²+z²/c²=1

 

Seti tupu/Empty set

Ni seti isokuwa na chochote kile.

 

Poligoni sawa/Equilateral Polygon

Ni poligoni yenye pande zote sawa.

 

Traiangu sawa/Equilateral triangle

Ni traiangu yenye pande zote sawa.

 

Nambari iveni/even number

Ni inteja inayoweza kugawika mara mbili.

 

Ekisiponenti/exponent

Katika ekisipreshoni x², x huitwa besi nayo 2 ikawa ekisiponenti.

 

Fankishoni ekisiponenti

Ni fankishoni f(x)=e²

 

Fakta/factor- Nomino

Ni nambari inayoweza kugawa nyingine sawasawa. Kwa mfano 7 ni fakta ya 28.

 

Fakta/factor- Kitenzi.

Ni kutafuta fakta za nambari Fulani.

 

Fakitorio/factorial

n! (inayotamkwa n fakitorio) ni sawa na kuzidisha nambari zote zilizo kati ya 1 na n. Kwa mfano 3!= 3*2*1 pale ambapo 3 ni n.

 

fomula/formula

Ni namna sifabia ya kuonyesha uhusian kati/baina ya kontiti/quantity mbili au zaidi.

 

Frakishoni/Fraction

Ni ekisipreshoni yenye umbo a/b.

 

Frikwenzi/friquenzi

Ni mara ambazo hali/nambari inatokeza baada ya muda Fulani.

 

Frastamu/Frustum

Katika umbile yambisi k.m. Piramidi au koni isokichwa pleni tako huwa sambamba na pleni juu.

 

 

 

 

 

   

Advertisements

April 9, 2006 - Posted by | Uncategorized

11 Comments »

 1. Sikujua kabisa mengi ya misamiati hii ya hisabati. Asante. Tunaelimika.

  Comment by ndesanjo | April 10, 2006 | Reply

 2. Nitakupa mawazo yangu ili kuchangia katika ujenzi wa kamusi hiyo.

  Comment by ndesanjo | April 10, 2006 | Reply

 3. Ile degree yako ya Kiswahili na Hisabati sasa inajidhihirisha bayana katika hili.Makene alikuwa na hoja siku moja aliponitwangia simu kuwa kuna haja ya blogu hizi kuwa na wataalamu wa fani anuai. Kumbe mpo isipokuwa hamvuni. Vuma mwanangu.

  Comment by john mwaipopo | April 11, 2006 | Reply

 4. Here are some links that I believe will be interested

  Comment by vicctoriorus76 | August 9, 2006 | Reply

 5. ninabashasha rojo rojo jinsi kamusi imenielimisha endelea vivyo hivyo mola awaangazie,ningependa mnitumie msamiati zaidi kwenye e-maile yangu .Asanteni sana

  Comment by moruri makori jared | February 7, 2007 | Reply

 6. ONLINE – DRUGSTORE!
  PRICES of ALL MEDICINES!

  FIND THAT NECESSARY…
  VIAGRA, CIALIS, PHENTERMINE, SOMA… and other pills!

  Welcome please: pills-prices.blogspot.com

  NEW INFORMATION ABOUT PAYDAY LOANS!

  Welcome please: payday-d-loans.blogspot.com

  GOOD LUCK!

  Comment by ModeBoada | November 2, 2007 | Reply

 7. Asante kwa kazi yako njema!
  Ebu, jaribu kuto maelezo ya maneno mengi yapatikayo ktika isibati!!

  Comment by Emmy Nya7 | September 10, 2008 | Reply

 8. Ningependa kuwaomba mnitumie msamiati zaidi kwenye e-mail yangu!Kazi hii ni nzuri!!

  Comment by Emmy Nya7 | September 10, 2008 | Reply

 9. kuna marekebisho mengi ya kiswahili hapa. nitaanza na jina la website yako…. kwa kiswahili sanifu, ni HISABATI, sio isabati angalia hapa:

  http://kamusi.co.tz/hisabati

  Comment by kamusi.co.tz | September 23, 2008 | Reply

 10. ndugu mtunzi,
  kweli nimefurahishwa na muamko wako unaolenga kupanua matumizi ya kiswahili katika hisabati na fizikia. Pamoja na pongezi hizo ningekushauri kupekua vitabu mbali mbali vinavyotumika nchini Tanzania katika kueneza elimu ya msingi (Primary School Education). Kuna maneno mengi ya kitaalamu ya kiswahili ambayo yangekusaidia: kwa mfano kanuni (formula),tarakimu (digit),pembe/pembetatu (angle/triangle),mshazali (diagonal), sambamba (parallel),nyuzi (degree), na mengine mengi. Umeanza jambo jema lakini si haba kwangu kunena kuwa “mtaka cha uvunguni sharti ainame” kwani ukita chako “chema” kipate “kuelea” basi huna budi “kiundwe”. Nasema tena hongera kwa mwanzo mzuri

  Comment by fidelis mutabazi | March 30, 2009 | Reply

 11. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea kupokea maoni na rai toka maeneo mbalimbali. Nakushauri kwamba yale maneno ambayo tayari kiswahili chake kipo usiyatohoe toka kiingereza utajitoa jasho na zahama ya bure. Halafu sio unatohoa toka lugha moja tu ya kigeni. Kiswahili kina utamaduni wake wa lugha na lafudhi. Endelea kutoa matunda maana si kila aliyeuotesha mwemba alikula mwenyewe bali walifaidika walokuja badaye. nawe endelea kwa moyo mkunjufu.

  Comment by Amska | November 14, 2016 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: