kwangila

Just another WordPress.com weblog

ELIMU YA KISASA INAMDANGANYA MWANAMKE WA KIAFRIKA?

Zama zile hakukuwa elimu hii tunayoipokea. Kungwi, shangazi na nyanya zetu walitwikwa mzigo wa kumuelekeza binti. Elimu kuu ilihusu namna ambavyo anaweza kuishi na mumewe katika ndoa na majukumu yake katika familia japo katika jamii ya waswahili binti alifunzwa pia kumfurahisha mumewe. (Rejelea Utenzi wa Mwanakupona.). Hivyo basi elimu ya msichana ilitofautiana pakubwa na ile ya mvulana.

Ni muhimu nitaje kwamba elimu hii ya kale kwa msichana haikutilia maanani mabadiliko katika gharama za maisha. Jamii zilikuwa na mali nyingi kuanzia mashamba, mifugo n.k. Hivyo basi , mwanamke hakutarajiwa kwenda nje eti kutafuta kazi. Iwapo ni chakula mwanamke aliingia shambani na kuchimbua mhogo. Iwapo ni moto, mwanamke hakwenda dukani kunua gesi, aliingia msituni na kuzoa tita la kuni.

Katika jamii ya kisasa, gharama ya maisha imepanda. Mashamba yamekuwa haba kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Vilevile maajilio ya tekinolojia na elimu ya kimagharibi imepelekea msichana kupewa elimu inayoenda na wakati. Lakini swali ni je sababu za kale za kumuelimisha binti zimebadilika au la. Iwapo zimebadilika zina madhara?

Kwa maoni yangu , nikidhani sababu hizi hazifai kubadilika. Elimu ya msichana inafaa kumwandaa kuwa mke bora zaidi kwa mumewe na jamii kwa jumla. Aidha ,anapoelimishwa binti anastahili kuhamasika zaidi kuhusu majukumu yake katika famila. Elimu hii haifai kamwe kumwelekeza msichana kuwa na fikra kwamba hana haja ya mwanamume katika maisha. Binti anapoelimishwa na kuwa Wakili baadaye hastahili kutumia nafasi hii kumea pembe. Huenda mumewe ni maskini wa elimu hivyo basi binti aliye na elimu hafai kamwe kumwona mumewe kama ganda la ndizi. Hastahili kamwe kutumia elimu aliyopata kudharau nafasi ya mumewe katika familia. Kama ilivyo utamaduni wetu waafrika jikoni huwa kwa mwanamke. Mara nyingi wanawake walioelimika wanatumia nafasi hiyo kuwapa zamu waume wao kusonga ugali, kutoa vitoto napkini, n.k. Ikizidi hawa walioelimika watawanyima waume zao haki ya kimsingi pia. Nina maana ya ngono. Baadhi ya wanawake walioelimika wamelishwa mawazo potovu kwamba wana haki ya kukataa kuridhia ngono. Elimu hii vilevile imepelekea wake za watu kuhudhuria vikao/sherehe  pasipo vibali au waume zao kujua wako wapi. Utaajabia kusikia baada ya kazi jioni , mwanamke alihudhuria sherehe ya bosi wake hoteli fulani pasi mumemwe kujua. Hali iliyompelekea kufika nyumbani usiku wa manane.  Labda nitapata makombora hapa kutoka kwa wanawake ambao wanaiona elimu hii inastahili kumpa binti uhuru wa kujifanyia maamuzi mwenyewe.

Ninawavulia kofia wanawake walioelimika na bado wanawapa waume zao heshima wanazostahili. Kuna wanawake Marais, Mawaziri, Maprofesa n.k. ambao huvua vyeo vyao na digrii zao wanapoingia nyumbani. Wakiwa nyumbani hutojua kuwa ni Mahakimu katika mahali pao pa kazi. Hutowasikia wakijibizana na waume zao wanapokatazwa kufanya jambo fulani. Aidha wanawake hawa wamejifunza unyeyekevu katika eilmu waliyoipata na unapowasikiza wanapozungumza utasikia wakiwasifu waume zao. Nilifurahia kusikia daktari mwanamke akimwambia mwanamke mwenzake kwamba ataomba ruhusa kutoka kwa mumewe ya kuhudhuria mkutano.

Iwapo dada mwafrika unadhamiria kutumia elimu kama chambo cha kumgandamiza mumeo umekosea. Wanaume walio wengi wana sifa moja kuu. Sifa yenyewe ni, kasoro za wake zao huwapelekea kutazama nje kuna nani. Haijalishi wake zao wana elimu kiasi gani.Ukimnyima mumeo ngono kwa madai eti una haki ya kukataa maanake umefunzwa hivyo , kesho utamsikia alilala kwa Fatuma. Ukikosa kumpikia chakula utamsikia hotelini na baadaye kwa Subira anayejua kwamba upishi ni jukumu lake.

Advertisements

April 6, 2006 - Posted by | Uncategorized

2 Comments »

  1. nionavyo mimi ni kuwa mambo huwa ni maelewano kama huko kwenye mitabendi moja na mwenziyo basi usitafute mahala pa kujificha eti kusema umesoma au vipi , sioni kama elimu inaweza kupotosha mtu namna hio , kama mtu ana tabia mbovu basi atachukuwa tu elimu kuwa kisingizio na kumbe kweli iko kwenye tabia zake .Na elimu au bila elimu wote wanawake na waume huwa wanatafuta visababu vya kutoroka shida zao

    Comment by maitha | April 8, 2006 | Reply

  2. uchambuzi wako ni mzuri lakini neno ngono lilivyotumika nafikiri si sahihi badala yake ungetumia tendo la ndoa nafikiri ndio sahihi ngono hufanywa na wale ambao hawajahalalishwa.

    Comment by mum | December 14, 2011 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: