kwangila

Just another WordPress.com weblog

VIJUSI MBONA TWAAVYA.

Swalingu naulizeni, mnipe jibu makini,

Ngono’zi twazichezani, na mimba twazitoeni,

Kitanda vunja jamani, mapenzi ni buriani,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Kijusi haki kahini, kibali kakupa nani,

Uhai kesha kihini, vituko hivi vya shani,

Bure kakupa manani, uhai nyima kwa nini,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Siambe huna mapeni, mavazi kwako pomoni,

Si’lize mwana talani, minofu wala sokoni,

Siambe ghali sahani, madodo toto mpeni,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Katoa tumbo kinyani, kadungwa sumu sindani,

Katoa tumbo kimbuni, kakata kichwa mwilini,

Katoa tumbo kinyani, katupwa mwana chooni,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Mamangu nakuulizeni, waraka kaandika lini,

Uhondo kawa lahani, kazuka mi kitandani,

Shakawa wazinyonyani, wapandwa kwako shambani,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Katupwa mi’ msituni, majibwa kanitafuna,

Katupwa jana chooni, viwavi nyama kapata,

Metupwa leo mitoni, viboko wote kafuata,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Ya mola kajua nani, kijusi huyu raisi

Ni siri yake maanani, balozi huyu kijusi,

Hakimu yeye Rabani, kijusi huyu ni nesi,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Muzae mwana karani, umupe tasa Halima,

Na mwana hana Mueni, alia wakilalama,

Na mwana usitupeni, peleka mama Fatuma,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Mwenyezi takulaani, rotuba shamba tatowa,

Unapopita njiani, we shoga mate tajawa,

Na kisha ya Firauni, kwa siri ndwele takuwa

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

 

Betizi zakutosheni, ya ziada jalizeni,

Machungwa yamo moyoni, kwa uno uhayawani,

Kijusi kizaliweni, mapanga sikitieni,

Shangazi swali yakini, kijusi mbona twaavya?

Advertisements

April 4, 2006 - Posted by | Uncategorized

3 Comments »

 1. Haya ndugu yetu, naona nawe ni mtu wa kushusha aya bin aya. Kumbe malenga hawatoki Tanzania tu. Moja ya faida za ninyi Wakenya mnaoblogu kwa Kiswahili ni kuwa mnavunjavunja mtazamo kuwa Wakenya hawajui Kiswahili. Mtazamo huu, sio tu wanao watu toka nje ya Kenya, bali hata Wakenya wenyewe. Nadhani kuna faida kubwa sana kuwa na taifa lenye watu wanaojua Kiswahili, kiingereza, na lugha za makabila.

  Comment by ndesanjo | April 5, 2006 | Reply

 2. nimeshukuru kuitembela blogu yako ewe mtandawazi.
  mashairi yako ni murwa kweli kweli.
  tueneze kiswahili katika ulimwengu huu wa blogu..
  shukrani..

  Comment by mhujumu | April 6, 2006 | Reply

 3. taibu! shairi safi kabisa kiswahili kienezwe

  Comment by michael kamau | June 19, 2014 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: