kwangila

Just another WordPress.com weblog

MISHAHARA YA WABUNGE INAUMIZA WANANCHI.

Bunge litahudhuriwa na wabunge iwapo mjadala utahusu nyongeza ya mishahara yao. Ijapo mijadala ya jinsi ya kupunguzia raia umaskini basi bunge litahudhuriwa na Kilemi Mwiria peke yake. Hawa 'waheshimiwa' wanajua kuzua mijadala kama vile 'Donde bill', 'Keter bill' n.k. lakini hamna yeyote ameshawahi kuzua mjadala wa 'kupunguza mishahara ya wabunge'.

Ni kosa na laana kubwa kuomba misaada kwa madai eti mnataka kupunguzia raia umaskini kisha badala yake mnajilimbikizia misaada hii kama nyongeza ya mishahara. Nchi inayotegemea misaada kama Kenya haifai kuwa inawalipa wabunge nusu milioni na zaidi. Huyu ni mbunge eti, ijapo waziri basi atapokea milioni mwisho wa mwezi. Haikosi ndio sababu madeni ya Kenya ni mengi kupindukia. Marekani yenyewe isiyokuwa na madeni haiwapi wanasiasa wake kiasi kama hiki cha pesa. Uingereza vilevile tumeelezwa kwamba mmoja wa wanasiasa wake huenda kazini kwa baiskeli.

Ijapo kuomba misaada hata akina Professa Kibwana na wenzake huvua uprofesa na kutia saini misaada hii kuja. Akilini mwao huwazia tu namna ambavyo misaada hii itawasaidia kupokea mamilioni ya pesa kila mwisho wa mwezi. Mradi mlipa kodi ambaye ni raia wa kawaida atalipa, mbona professa ajisumbue kuhakiki athari za mikopo kwa raia wa kawaida? Mirundiko ya madeni kama haya ndiyo yamepelekea ushuru kupanda, na serikali kuanza kuwalazimisha wafanyibiashara kutumia mitambo ya kurekodi mauzo yao.

Nikidhani huu unastahili kuwa mkataba kati ya raia na serikali ijayo mwaka wa 2007. Kwamba tutawapa kura tu iwapo watatuahidi kuwa watapunguza mishahara yao. Hivi ndivyo wakenya wanawaambia akina Uhuru, Kalonzo, Kibaki, Raila, Ruto na Balala. Sijajua sababu ya mwalimu kupokea elfu kumi kisha mbunge kupokea milioni kama mshahara. Je ina maana mbunge hula dhahabu huku mwalimu akila sukuma wiki? Je ina maana kinyesi cha mbunge ni tofauti na cha mwalimu? Je ina maana mbunge huishi mwezini huku mwalimu akiishi duniani?

Advertisements

April 1, 2006 - Posted by | Uncategorized

2 Comments »

  1. Tanzania nako ni kama Kenya. Wabunge huwa hawasiti kujadili mishahara yao mara tu wanapoingia bungeni. Hakuna mbunge anayethubutu kudai kuwa wasiongozewe mishahara na marupurupu kwakuwa Tanzania ni nchi masikini na kuna wafanyakazi wengine kama walimu ambao wana mishahara duni au kuna wazee ambao hawajalipwa viinua mgongo vyao. Asilimia kubwa ya wabunge wanachukua cheo hiki kuwa sio utumishi bali ni njia ya kujipatia mali.

    Comment by ndesanjo | April 1, 2006 | Reply

  2. more on base

    Comment by jack | January 9, 2007 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: