kwangila

Just another WordPress.com weblog

HAMNA UBAKAJI KATIKA NDOA.

Mitindo mibaya ya kimagharibi inanyemelea jamii za Kiafrika kwa kasi
mno. Wanawake hasa walioelimika wameambukizwa ndwele na wanaharakati
wanaodai kwamba wanatetea haki za mwanamke. Nikiegemeza mjadala wangu
katika misingi ya dini ya Kikristo ni kwamba haikuwa mapenzi ya MWENYEZI
MUNGU mwanamke kusema kwamba anadai haki zake. Aidha Biblia takatifu
inasema mwanamke anastahili kuwa mnyenyekevu kwa mumewe. Naye mwanamume
ameshauriwa kumpenda mkewe.

Panapo unyenyekevu na mapenzi basi hamna dhana ya ubakaji. Iwapo bwana
ana nyege mkewe anastahili kuwa tayari kumkidhia haja zake. Panapo
mapenzi basi mume atajua kwamba mkewe si panya kiasi cha kujifungua watoto
kila kukicha. Mapenzi vilevile yatapelekea mume kutambua kwamba mkewe
anaugua hivyo basi itakuwa kumuumiza iwapo atadai ngono. 

Dhana hizi za mwanamke aliyeolea kudai kwamba alibakwa na mumewe ni
potovu na zinastahili kupingwa kwa vyovyote vile. Haikosi ndio sababu
wanaharakati hawa wanadai mume na mke ni viumbe sawa. Haiwezekani abadan
katan! Mume aliumbwa kwanza Biblia inasema kisha MUNGU akaona kwamba ipo
haja ya huyu mwanamume kuwa na msaidizi. Hivyo nafasi ya mwanamke
katika jamii inayoongozwa na maadili ya dini ya Kikristo ni ya msaidizi.
Haifai kamwe mwanamke kudai ukurugenzi katika familia.

Ukweli ni kwamba iwapo wanawake wataendelea kubugia sera za magharibi
bila kuzihakiki na kuzipigia maswali basi watajioa wenyewe. Waume zao
watawataliki na walioelimika wataozea nyumbani mwa mama zao.
Watakaobarikiwa ni wale wasio na elimu na wanaotambua uanauke ndio nini. 

Advertisements

April 1, 2006 - Posted by | Uncategorized

13 Comments »

 1. Nakubaliana nawe kabisa kuhusu suala la unyenyekevu na upendo kuwa ndio msingi wa ndoa. Lakini sikubaliana na uchambuzi wako ambao ili mtu akubaliane nawe lazima basi awe anakubali kuwa hadithi ya wayahudi ya adamu na hawa walioumbwa miaka kama miaka 5000 iliyopita ni ya kweli.

  Kingine ni kuwa wakati unataka waafrika kuwa makini kwa kutoiga mambo toka nje ya Afrika bila kuhoji, unatumia hadithi za kidini toka nje ya Kiafrika kujenga hoja yako ya kuwa mwanamke ni msaidizi. Kwanini tujenge imani kuwa jambo likiwa ndani ya biblia basi lina nguvu ya kuwa mwanga wa maisha yetu hapa duniani na sio simulizi zilizoko kwenye imani zetu za jadi?

  Kati ya mambo mengi ambayo mimi binafsi sikubaliani nayo yaliyoko ndani ya biblia ni jinsi mwanamke anavyochukuliwa. Paulo (wako wanaomwita Mtume) anasema kuwa mwanamke hana haki ya kufungua mdomo kanisa. Haruhusiwi kuongoza ibada au kufundisha. MWanamke akiwa na swali lolote, Paulo anatuambia, anabidi asubiri hadi akirudi nyumbani amuulize mkewe. Biblia hiyo inatuambiwa kuwa aliyeko mbinguni ni “baba” na sio “mama” ndio maana wakristo wana sala wanaiita Sala ya Bwana isemayo: Baba yetu uliye mbinguni….
  Historia ya jamii ya wakati ule biblia ikiandikwa inatuonyesha kuwa mfumo dume ulikuwa umefikia kilele. Ni mfumo dume huu huu ambao unauona hata unaposoma kitabu kama Kurani ambapo muislamu anaambiwa kuwa mke akikosea kuna mambo mawili ya kufanya: kuacha kulala naye kitanda kimoja au kumpiga.
  Hapo unajiuliza, je mume akikosea? Nilimuuliza muislamu mmoja kule Ohio akaniambia kuwa mume akikosea ataitiwa kikao cha wazee ila mwanamke atapigwa!

  Tuendeleze mjadala.

  Comment by ndesanjo | April 2, 2006 | Reply

 2. Kyeu,
  Nafurahia ujio wako. Nimekuta maoni yako nyumbani kwangu. Sikuwepo kwa muda fulani.
  Nafurahi kusikia kuwa u mwalimu! Furaha ilioje!
  Nyumbani kwako kunapendeza sana. Shelfu zako zimesheheni ukwasi wa mistari ya ufahamu. Kazi nzuri sana.
  Nimepitia kukukaribisha. Nadhani ntatoa maoni nikija mara nyingine. Ninahangaika na makaratasi, yananizua kutembea tembea ipasavyo. Nitakuwa hapa baadae kidogo kama sio kesho.
  Masuala unayozungumza yamenipa changamoto sana mwalimu. Hongera!

  Comment by Bwaya | April 2, 2006 | Reply

 3. Samahani kidogo,
  kiunganishi cha mwaipopo kinamatatizo. Nadhani nyumba hiyo alishahama siku nyingi. Jaribu kubadili kibao kielekeze “www.mwaipopo.blogspot.com”

  Comment by Bwaya | April 2, 2006 | Reply

 4. Nakubaliana nawe Mtandawazi, ila pia nahimiza upendo na heshima kati ya mume na mke. Kristo mwenyewe alitupa mfano unaostahili, ama wasemaje?
  http://mkenyamdadisi.blogspot.com

  Comment by mdadisimkenya | April 2, 2006 | Reply

 5. Ni wazi kabisa kuhusu tatizo la kimapokeo miongoni mwa nchi na watu wetu wa Afrika kutokana na tunaliliona au kulisikia kutoka magharibi.Utamaduni na mila zetu zinazidi kuzikwa siku baada ya siku.Hii ni vita ambayo ni lazima tuipigane kwa udi na uvumba na bila kuchoka.Cha muhimu sana katika hili ni upendo..panapo upendo kisha tukachanganya na imani kwamba kilicho chetu ni kizuri kuliko chao basi tutafika.Hatuhitaji kupigana wala kutoana ngeu.Uvumilivu,maelewano,upendo na kusamehe nadhani ni misingi muhimu sana ambayo wazee wetu walituwekea.Usawa wa kibinadamu usichanganywe na usawa wa nafasi zetu katika jamii.Kama anavyopenda kusema Makene,cheza karata yako.

  Comment by Jeff Msangi | April 3, 2006 | Reply

 6. Kyeu,
  Umesema sawa kabisa. Sidhani kama inawezekana binadamu asiathirike na imani yake katika matendo au matamshi yake. Na kweli imani zimejazana dunia hii. Mtu mmoja aliwahi kusema dunia ina imani na dini nyingi za kutosha kutufarakanisha ila sio za kutufanya tuishi kwa amani!
  Nimeenda pembeni, bila kuwa na woga wa kusema vitabu hivi vinavyoonekana machoni kwa wengi kuwa vina maneno ya mungu (zaidi ya vingine!) vimejaa falsafa za mfumo dume uliopita kiasi…inanifanya kumshuku huyo mungu. Mungu anayeweza, kwa mfano, kusema (kama ilivyo kwenye kitabu cha Mwanzo) kuwa mwanamke amelaaniwa MILELE kwakuwa alikula tunda na kuwa atakuwa chini ya mamlaka ya mwanaume daima. Naamini kuwa wanaume na wanawake tuna wajibu tofauti (kwenye masual fualani) na pia nafasi tofauti katika jamii na hata kwenye familia. Lakini hili suala la eti “mwanaume atakutawala daima.” Sioni upendo hapo ila naona mtawala na mtawaliwa.

  Mungu huyo huyo aliyekwenda kwa Waisraeli na kuwaambia wavamie maeneo mbalimbali wakiwa njia kuelekea “nchi ya ahadi” na eti wakishavamia maeneo hayo waue kila mwanaume na mwanamke ambaye sio bikira na wale bikira wawachukue kuwa wake zao…kama mauaji ya halaiki na uchu dhidi ya mwili wa mwanamke bikira sio haya…basi niambiwe.

  Kuhusu uhalali wa dini fulani. Nadhani tunaweza kujifunza toka tamaduni zetu. Tazama mfano huu: Mimi ni Mchagga. Ingawa imani ya Kichagga ni tofauti na ya Kimasai au ya watani wetu Wapare, Wachagga hatusemi kuwa eti Wapare na Wamasai (kwakuwa wana manabii au mafunzo tofauti ya kiimani na kiroho) wataenda motoni. Tunasema kuwa wana imani tofauti ila sio imani potofu. Sasa kwenye dini hizi za kuja ni kuwa kama wewe ni muislamu, basi mkristo ana imani potofu na anakwenda motoni. Na kama wewe ni mkristo na kuna mtu mwingine ana imani tofauti na yako sio kuwa imani ya huyo mtu ni tofauti ila ni tofauti na potofu. Kuna somo fulani hapa tunapaswa kuchukua toka kwenye mitazamo ya jadi.

  Lakini jambo kuu nililotaka kusema ni kuwa kama tutakuwa tunataka tafsiri ya kuwepo au kutokuwepo kwa tendo la kubaka ndani ya ndoa itolewe katika darubini ya utamaduni wetu, basi hakuna haja ya kutumia mifano ya kitabu ambacho kinasema kuwa kuna mataifa 12 ya wateule wa mungu na makabila hayo wakikuyu, wasambaa, wadigo, washona, n.k. hawapo. Hakuna sababu ya kutumia kitabu toka kwenye hadithi za tamaduni nyingine wakati nasi tuna hadithi na simulizi zetu. Si ndio?

  Comment by ndesanjo | April 6, 2006 | Reply

 7. Ubakaji si ni kumshurutisha mtu kufanya ngono kwa nguvu na vitisho sio? Ni suala la nani mwenye nguvu za kumkandamiza mwengine atake asitake.
  Kumshurutisha mtu kufanya ngono bila ridhaa mie naona si sawa, iwe ndani ya ndoa au nje. na kama mmoja wa walio kwenye ndoa hiyo anamnyima mwezie unyumba kila wakati hata mwenziwe akizidiwa – basi nini maana ya ndoa?
  ikishindikana kabisa, ndio ishabidi, mmoja itabidi aanze, sidhani kama kuna ulazima wa kubaka.

  Comment by mwandani | April 6, 2006 | Reply

 8. Wake wanaowanyima waume zao kufurahia unyumba, mara nyingi wana sababu nyingi ya kufanya hivyo. Hakuna mwanamke ambaye anaweza kuwa ‘baridi’ kwa mumewe bila sababu. Kuna wanaume ambao kila siku lazima anataka ‘vitu’ vya mkewe na hataki kujua kwamba, nyakati zingine mke wake ana hedhi au anaumwa na tumbo kwa sababu ya hedhi. Pia, mwanamke akishuku kwamba mumewe anatembea na wanawake wengine, bila shaka, hatahisi kufanya mapenzi naye.
  Isitoshe, mwanamke anapofikia umri wa mika 50 na kuendelea, hali yake ya mwili inabadilika kwa kuwa hapati hedhi tena.
  Mume anapohisi kwamba, mkewe hataki kuonana naye kimwili, afaa achunguze ni nini haswa kiini cha kukataliwa.
  Hali ya kurukiana na kuraruliana chupi eti kwa sababu umemlipia mahari mkeo, si nzuri kabisa. Mume hana haki kumlazimisha mkewe kufanya naye mapenzi. Anatohitajika kufanya ni kuzungumza naye na ikishindikana , watafute usaidiszi kwa wataalam wa ndoa.

  Comment by dorothy jebet | April 13, 2006 | Reply

 9. Doh! Dorothy umenielimisha hapa!

  Comment by mwandani | April 17, 2006 | Reply

 10. Kwa kewli siki hizi hawa wanawake wasomi wanaleta shida katika jamii hasa ndoa zao,wanameza sana haya mambo ya Gender na kuyafanyia kazi kama jinsi yalivyo katika maandishi pasipo kuangalia nini sababu hawa wazungu wanadai hiyo,kumbuka hawa wazungu wanasema hata Biblia takatifu ina gender imbalance jamani hii ni laana,wamama na akida dada kuweni makini tuenende kwa misingi ya kibiblia,fahamu wamama wengine wanaoadvocate sana gender wengine hawajaolewa au wameachana na wume zao au waume walifariki na walio wengi hao wamama hawamjui vizuri Yesu na Biblia kwa ujumla

  Comment by Nsangalufu | May 7, 2008 | Reply

 11. Ahsanteni sana ndugu wachangiaji.Kila mtu anajitahidi kadri ya uwezo wake kuweka Elimu yake kutetea anayo ona sawa kwake.Amma Kweli Wahenga wamesema Akili ni Nywele Kila Mtu ana Zake.Kama vidole vitano ya kiganja havipatani hivyohivyo maoni na elimu pia haiwezi kuapatana.Lazima itatofautiana.KUHUSU SUALA YA MUME KUMBAKA MKE.
  NAMI NAPENMDA KUCHANGIA KAMA IFUATAVYO.
  MWANZILISHI WA NDOA NI MWENEYZI MUNGU.Kwa hiyo ndoa ni Ahadi kati ya M/Me na M/Mke.kila mmoja anajukumu la kuheshimu Ahadi hiyo.mwanaume anaye mwoa M/Mke kwa njia ya kisheriah na kumlipa MAHARI.Na M/Mke akishapokea hapo tayari Tupu ya M/Ke aliyepokea mahari inakuwa halali kwa M/me aliyemwoa.
  kwahiyo M/Mke hana haki kumyima unyumba mume wake wakati wowote iwe mchana ua usiku.Mwanaume anayo haki kamili kustarehe na mwili wa mke wake wakati wowote atakayo.Au siyo?
  Siku hizi kuna wanawake waliokosa mwongozo wa KIROHO wamekuwa kero mkubwa kwa wanaume zao.Pindi waki itwa kutimiza haja ya mume zao wao hutoa sababu za kipuuzi kama
  wamechoka,wanakazi,wamekwisha oga,na mengi mengineo.
  Mtume wa Waislamu amesema Mwanamke yeyote akiitwa na mume wake kukidhi haya yake kitadani,na mke akimkatalia bila udhuru za sheria kamwa kuwa katika siku zake n.k.basi mke huyu Malaika wanamlaani hadi asubuhi na katika hadithi nyingine analaaniwa na Malaika mpaka mume wake amridhie.
  Sasa swali waweza kuingia kichwani nayo ni:
  KWANINI MTUME WA WAISLAMU AMETILIA MKAZO JAMBO HILI NAMNA HII?.
  Jibu la swali hii kwa ufupi napenda kuweka hivi sote tunafahamu wanadamu wote kimaumbile tumetofautiana sana.
  Amma Siyo?.
  kwahiyo kuna wanaume wanaweza kuvumilia wakikosa unyumba na kuna wanaume kamwe hawawezi kuvumilia.
  Je! hii ni kweli au si kweli?.

  Sasa napenda ku uliza Ki-Ungwana niambieni huyu mwanaume asiye weza kuvumilia afanye nini kati ya haya matatu?
  1.Ajitese mwenyewe kwa kuvumilia hivyohivyo
  2.Aende kwa malaya na kununua UKIMWI au
  3.AMBAKE MKE WAKE ANAYEMYIMA UNYUMBA BILA SABABU ZA KISHERIAH YA DINI YAKE?.

  SASA KUMWIGILIA MKE KWA KUTUMIA NGUVU TUTA ITA UBAKAJI?
  MIMI NAAMINI KUMBAKA MWANAMKE AWE BINTI AU MKE WA MTU NI KOSA LA JINAI,LAKINI MUME KUMWINGILIA MKE WAKE MWENEYWE KWA NGUVU NIAMBIENI NAYO ITAKUWA KOSA LA JINAI?

  MAJIBU YA HAYA MASWALI JIBUNI WENYEWE.

  NATARAJI NILIYOCHANGIA YATAKUWA YENYE MANUFAA JAPO KIDOGO KWA WALE WENYE TAFAKRI NZURI NA KUPENDA MAADILI MEMA.

  Comment by Ibrahim | August 24, 2008 | Reply

 12. Kwa kusema ukweli, baadhi ya wanaume wana tabia mbaya mno. Mtu akishalewa anafika nyumbani saa nane za usiku akiwa ananuka kama samaki ambaye hajapikwa. Mume huyo huyo, atapampata mkewe akiwa amelala na atamuamsha akidai ‘haki’ yake. Hebu jiweke katika hali hii ya mwanamke mwenye mume sampuli hii! Wakati huo hata kama unampenda mumeo, tamaa ya mapenzi huwa imechomoka dirishani kwa sababu ya harufu mbaya mdomoni na soksi zake. Hakuna mwanamke anayependa kujaamiana na mwanaume anayenuka. Mume akishataka, hataki kujua kama umeudhishwa na chochote; atakurukia na kukumenya hata upige nduru. Katika kule kusukumana na kujaribu kukwepa mume, mwanamke atadai kuwa hakutaka kufanya tendo hilo na mumewe. Kuhusiana na hayo, nawasihi sana wanaume wawe wakijali maslahi ya wake zao ili kitendo hiki kisiwe chanzo cha ndoa kuvunjika. Mbona wewe mwanaume ukifika kutoka ulevini hutaki kusugua meno na kuosha miguu yako kabla ya kumparamia mama watoto? Hata kama ulilipa mahari ya ng’ombe 60 na kuku wawili, hiyo si kibali cha kumkosea heshima mkeo. Wanawake hupenda usafi kila mahali walipo, hata kitandani. Bibilia pia huenzi usafi.

  Comment by Dorothy Jebet | September 15, 2008 | Reply

 13. You are right brother.

  Islam says the same thing, Thank you for this nice post.

  Comment by sekenke | December 9, 2015 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: