kwangila

Just another WordPress.com weblog

KENGEN YAUZA HISA SASA.

Ndugu zangu Wakenya wana habari kwamba KENGEN( Shirika pweke la usambazaji umeme Kenya) inauza 30% ya hisa zake kwa umma. Kwa Wakenya ni shilingi 11.90 za Kenya kisha kuna bei ya raia kutoka TZ na Uganda ambayo ni nafuu kiasi kuliko ya wageni kutoka nchi zingine.

KENGEN ni mojawepo ya mashirika ambayo hadi sasa yanamilikiwa na serikali. Historia inaonyesha kwamba KENGEN imekuwa ikipata faida tangu ilipoanzishwa. Hii ni mara ya kwanza tangu Kenya kupata uhuru Serikali kujaribu kuwapunguzia raia umaskini kwa kuweka mazingira mufti ya uwekezaji.

Hisa zimeanza kuuzwa tarehe 20 machi na itafungwa tarehe 14 Aprili. Panapo majaliwa huenda mwisho wa mwaka thamana ya hisa hizi itakuwa imepanda hadi kufikia zaidi ya shilingi 50 za Kenya. Hivyo itakuwa faida kwa yeyote ambaye atakuwa amewekeza.

Kwa WaTZ mnaweza kuwatuma jamaa zenu Kenya katika Kenya Commercial Banks ili waweze kuwanunulia hisa kabla ya kipindi kufungwa. Iwapo mtahitaji habari na usaidizi zaidi niko tayari kuwapa maanake tunaelekea kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Advertisements

March 28, 2006 - Posted by | Uncategorized

2 Comments »

  1. Haya ni maendeleo ya kuvutia mno na nataraji hatua hii itaimarisha shirika la KenGen na pia kuboresha huduma kwa wateja.

    Nina swali…kama kila hisa inauzwa 11.90Ksh, inahitajika kununua ngapi (kiasi cha msingi zaidi) ili kuweza kuwa mwenye hisa imara?

    Comment by akiey | March 28, 2006 | Reply

  2. Karibu bwana mkubwa katika gazeti Tando.

    Comment by Egidio Ndabagoye | March 29, 2006 | Reply


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: