MAREKANI INAVYOFADHILI VITA BARANI AFRIKA.
Habari kwamba Marekani inawafadhili mibabe wa vita nchini Somalia inastahili kuwaamsha viongozi wa bara la Afrika na ulimwengu kwa jumla. Tangu 1992 hakujakuweko serikali nchini Somalia baada ya nchi hiyo kusombwa na mizozo ya kikabila. Serikali ya Siyad Barre ililazimika kung'atuka baada ya baadhi ya mibabe wa kivita kuziongoza jamii zao dhidi ya serikali. Hali hii ilipelekea Wasomali wengi kukikimbilia nchini Kenya. Hivi sasa kuna zaidi ya Wakimbizi 100,000 katika kambi ya Wakimbizi ya Daadab Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Ni muhimu kutaja kwamba katika zile harakati za vita vya kikabila, Wasomali wengi waliuawa, wengine kubakwa , wengine walitafunwa na wanyama pori na zaidi wengine wamekuwa walemavu wa kudumu.
Katika mwaka wa 2004 serikali ya mpito iliundwa rais wake akiwa Rais Abdullahi Yusuf. Haya yote yalifanyikia Nairobi maanake pilipili ilikuwa imetapakaa kote mjini Mogadishu na miji mingine. Hata hivyo ilibidi Serikali ya Adullahi kuhamishwa hadi mji salama kiasi wa Johar nchini Somalia baada ya shinikizo kutoka jamii ya kimataifa. Serikali hii haingeweza kupata makazi Mogadishu maanake mibabe wa vita wenye silaha kali wangali wanathibiti kila kitu jijini Mogadishu. Asilimia kubwa ya serikali hii ya Abdullahi ni mibabe wa kivita ambao ni sugu hata hivi leo. Hawakubaliani kwa asilimia 100 na sera zinazopitishwa na bunge.
Licha kwamba serikali ipo sasa, Abdullahi amedai kwamba Marekani inawafadhili mibabe wa kivita badala ya kuifadhili serikali kupitia taasisi zinazostahili kutumika. Alisema haya nchini Uswidi na zaidi akasema kwamba Marekani haiko radhi kuona kwamba nchi hii ya Somalia ina amani. Aidha ufadhili wanaopata mibabe hawa unawapelekea kuwa sugu zaidi kiasi kwamba hawasikii lolote analosema Abdullahi. Hawatambui katu kwamba kuna rais, kazi yao ni kushirikiana na Marekani kuongeza vita nchini Somalia kwa madai eti wanayawinda makundi ya Ki-Alqaida. Bwana wao sasa ni Marekani bali sio Abdullahi.
Mataifa mengine barani Afrika ambayo yamesombwa katika mizozo barani Afrika ni yale yenye mafuta na madini adimu duniani. Mifano ya mataifa haya ni Sudan, Nigeria, Congo, n.k. Nitarejelea Sudan pekee katika mjadala huu. Je Marekani inachangia vipi katika mzozo wa Darfur nchini Sudan?
Eneo la Darfur linajulikana kama lenye mafuta na kwa muda mrefu limekuwa kitega uchumi cha serikali ya Sudan. Marekani haifurahishwi na uamuzi wa serikali ya Sudan kuuzia mafuta mataifa mengine mbali sio Marekani. Marekani ilipotaambua hili, iliamua kumtumia John Garang kuipiga vita serikali. Marekani iliwahami wanajeshi wapinzani wa SPLA na SPLM walioongozwa na John Garang. Swala kuu lilikuwa Sudan kusini iwe taifa huru. Kwa njia hii Marekani ingeweza kushauriana na serikali ya John Garang (ambaye angekuwa rais wa Sudan Kusini )bila kuomba ruhusa kutoka kwa el-Bashir. Hta hivyo Garang aliaga katika ajali ya ndege pindi tu mkataba ulipotiwa saini jijini Nairobi. Hali hii ilipelekea makamu wake Savar Kiir ambaye hana elimu yoyote kuchukua hatamu za uongozi. Kubuka John Garang alikuwa Daktari kando ya kuwa mwanajeshi.
Katika mifano hii miwili ya Somalia na Sudan, ni wazi kwamba kuwepo mizozo barani Afrika kunafadi Marekani. Wanafaidika na wakimbizi maanake wanawahamisha baadaye hadi nchini Marekani kufanya kazi za kishenzi. Habari nilizopokea hivi juzi ni kwamba Marekani inawahamisha wakimbizi zaidi ya 30,000 kuja Marekani kufanya kazi. Nilidhibitisha haya nilipowazuru Wakimbizi wa Kisomalia ambao wanaishi Providence nchini Marekani. Aliyesema utumwa ulitoweka ungalipo hadi hivi leo hasa katika uhusiano wa Marekani na Mataifa yenye mizozo barani Afrika.
Faida ya pili wanayolenga Wamarekani ni kutokana na kuwepo mizozo ni mafuta kwa ajili ya magari yake, ndege na kupasha vyumba joto wakati wa baridi. Unaposikia Marekani inatafuta mafuta barani Afrika imebeba silaha kwa mkono wa kushoto ili kuwapa wapinzani wa serikali endapo itanyimwa mafuta. Si eti Marekani haina mafuta yake, bali wanahifadhi rasilimali zao kwanza, watumie visima vya ulimwengu kisha warudie kuchimba vyao visima vya ulimwengu vinapokauka. Hii ndiyo sababu ninashuku kushuka mizozo katika mataifa yanayoipa Marekani leseni ya kuchimba visima nchini mwao. Ni wazi kwamba baada ya mataifa ya mashariki ya kati kutambua ushetani wa Marekani, yameanza kukatiza kiasi cha mafuta yanayokwenda Marekani. Halli hii inapelekea Marekani kuanza kuchimba mafuta barani Afrika. Hii ni dalili ya mizozo zaidi barani Afrika siku za usoni.
-
Recent
- MAREKANI INAVYOFADHILI VITA BARANI AFRIKA.
- MISHAHARA YA WABUNGE KENYA: WIZI! WIZI! WIZI!
- SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI.
- UBAKAJI: NJOKI NDUNG’U ANAFICHA HABARI FULANI.
- MADHARA YA KUWEPO SARAFU AINA MOJA AFRIKA MASHARIKI.
- KUNA HATARI YA KALONZO MUSYOKA KUWA RAIS?
- NAMNA YA KUPIMA UBORA WA MAISHA.
- KIFO NI NINI?
- KITOTO CHA MAREKANI KINASAFIRI ULIMWENGUNI ZAIDI YA MHADHIRI CHUONI AFRIKA.
- KUTOJUMULISHA MIKOPO YA WAFADHILI: HEKO SERIKALI
- MBONA MAREKANI NA UINGEREZA ZINAINGIA TANZANIA BILA BREKI?
- KAMUSI YA ISIBATI
-
Links
-
Archives
- May 2006 (2)
- April 2006 (14)
- March 2006 (12)
-
Categories
-
RSS
Entries RSS
Comments RSS