KAMUSI YA ISIBATI
Kama mwalimu wa Isibati nimeanza kutayarisha kijikamusi cha Isibati kwa Kiswahili. Nawaalika wataalamu wa Isibati kuihakiki kijikamusi hiki kadri ya uwezo wao. Nimelazimika kuswahilisha msamiati mwingi maanake hivi sasa sina suruali, inanibidi niazime kutoka kwa jirani kabla ya kupata suruali yangu. Ongeza visawe, punguza au zua mjadala utakaofanikisha mradi huu. Kamusi yenyewe i hapa chini.
KAMUSI YA ISIBATI
Kiselelisheni/Accerelation.
Namna ambavyo velositi hubadilika na wakati.
Ekwishoni Ajebura (Algebraic Equation)
Ni ekwishoni yenye umbo la f(x)=0: pale ambapo f ni Polinomio
Otitudi(Altitude)
Otitudi ya traiango ABC ni mstari kutoka vatekisi moja ya traiango ile hadi kwenye k.m Vatekisi A. Mstari huu hugawa
Mstari BC wa traiango ile kwa vipande sawa.
Ango(angle)
Mistari au pleni mbili zinapokutana kinachoundwa ni ango.
Wastani wa Kiarithimetiki/Avareji(Arithmetic Mean/Average)
Ni mgao wa hesabu ya vitu na idadi yake. K.m. iwapo thamana ya vitu ni ‘m’ na idadi ya vitu vile ni ‘n’ basi Avareji yake ni m/n.
Besi.(Base)
Katika ekipreshoni xⁿ , X ni besi huku y ikiwa ekisoponenti.
Namba bainari.(Binary number)
Ni nambari yenye besi namba 2
Baisekiti.(Bisect)
Ni kugawanya mara mbili. Vipande view sawa.
Biti.(Bit)
Hii ni dijiti bainari
Baiti.(Byte)
Ni kiwango cha memori kinachohitajika kuwakilisha karakita moja katika tarakilishi. Idadi yake huwa ni bit inane.
Ango Kati. (Central Angle)
Ni ango iliyo kati ya rediasi mbili.
Khodi.(Chord)
Ni mstari unaounganisha pande mbili za kavu Fulani.
Duara/ Sako. (Circle)
Umbo mzunguko ambalo sehemu zake huwa na urefu sawa kutoka sehemu iliyo kati.
Koni Duara. (Circular cone)
Ni koni ambayo tako
lake
ni duara.
Sakamusenta. (Cicurmcenter)
Sakamusenta ya traiango ni sehemu kati ya duara ilyochorwa ndani ya traiango ile.
Koefishienti.(Coefficient)
Ni konsonanti ambayo huzidishwa na kibadiliki Fulani katika polinomio.K.m. katika Polinomio X²+3X+7, Koefishienti ni 1, 3 na 7.
Ango Komplimentari. (Complimentary angles)
Hizi ni ango ambazo jumla yazo ni 90°
Nambari tata. (Complimentary angles).
Ni jumla ya nambari halisi nay a kufikirika. Km 3+4i pale ambapo i=√-1.
Konikevu. (Concave)
Umbo lililopindika ndani.
Maumbo kongurenti.(Congruent figures)
Ni maumbo ya kijometriki yanayolingana kwa ukubwa na umbo.
Kubu.(Cube).
Ni umbo yambisi lenye mistari sita inayolingana kwa urefu na kufungamana.
Ekwishoni kubiki.(Cubic equation)
Ni ekwishoni polinomio ya digrii 3
Dekagoni.(Decagon)
Ni polinomio yenye pande 10.
Nambari nukta. (Decimal number)
Ni nambari iliyoandikwa kwa kutumia besi 10.
Digrii.(Degree)
Digrii ya umbo lolote lile lenye vibadiliki ni ekisiponenti ya variabo/kibadiliki kile. K.m digrii ya 7X³ ni 3.
Dinomineta.(Denominator)
Atika nambari mgao x/y, x huitwa numereta nayo y ikatwa dinomineta.
Dayagono.(Diagonal)
Katika poligoni mstari unaounganisha vatekisi moja na nyingine isokuwa karibu huitwa dayagono.
Dayamita/Diameter
Katika umbo-duara, dayamita ni mstari unaopitia katikati mwa duara ile.
Dijiti/Digit
Ni nambari zifuatazo: 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9
Divaisa/Divisor
Katika nambari mgao a/b, a huitwa dividenti ilihali b ikawa divaisa.
Dodekagoni/Dodecagon
Hii ni Poligoni yenye pande 12.
Dodekahiduroni/Dodecahedron
Ni umbo yabisi/solid yenye nyuso 12.
Domeni/Domain
Domeni ya fankishoni f(x) ni mfululizo wa thamana ambazo x imepewa.
Elipsi/Ellipse
Ni umbo pleni ambalo ekwishoni yake ni x²/a²+y²/b²=1
Elipusoidi/Ellipsoid.
Ni umbo yambisi ambalo ekwishoni yake ni x²/a²+y²/b²+z²/c²=1
Seti tupu/Empty set
Ni seti isokuwa na chochote kile.
Poligoni sawa/Equilateral Polygon
Ni poligoni yenye pande zote sawa.
Traiangu sawa/Equilateral triangle
Ni traiangu yenye pande zote sawa.
Nambari iveni/even number
Ni inteja inayoweza kugawika mara mbili.
Ekisiponenti/exponent
Katika ekisipreshoni x², x huitwa besi nayo 2 ikawa ekisiponenti.
Fankishoni ekisiponenti
Ni fankishoni f(x)=e²
Fakta/factor- Nomino
Ni nambari inayoweza kugawa nyingine sawasawa. Kwa mfano 7 ni fakta ya 28.
Fakta/factor- Kitenzi.
Ni kutafuta fakta za nambari Fulani.
Fakitorio/factorial
n! (inayotamkwa n fakitorio) ni sawa na kuzidisha nambari zote zilizo kati ya 1 na n. Kwa mfano 3!= 3*2*1 pale ambapo 3 ni n.
fomula/formula
Ni namna sifabia ya kuonyesha uhusian kati/baina ya kontiti/quantity mbili au zaidi.
Frakishoni/Fraction
Ni ekisipreshoni yenye umbo a/b.
Frikwenzi/friquenzi
Ni mara ambazo hali/nambari inatokeza baada ya muda Fulani.
Frastamu/Frustum
Katika umbile yambisi k.m. Piramidi au koni isokichwa pleni tako huwa sambamba na pleni juu.
10 Comments »
Leave a comment
-
Recent
- MAREKANI INAVYOFADHILI VITA BARANI AFRIKA.
- MISHAHARA YA WABUNGE KENYA: WIZI! WIZI! WIZI!
- SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI.
- UBAKAJI: NJOKI NDUNG’U ANAFICHA HABARI FULANI.
- MADHARA YA KUWEPO SARAFU AINA MOJA AFRIKA MASHARIKI.
- KUNA HATARI YA KALONZO MUSYOKA KUWA RAIS?
- NAMNA YA KUPIMA UBORA WA MAISHA.
- KIFO NI NINI?
- KITOTO CHA MAREKANI KINASAFIRI ULIMWENGUNI ZAIDI YA MHADHIRI CHUONI AFRIKA.
- KUTOJUMULISHA MIKOPO YA WAFADHILI: HEKO SERIKALI
- MBONA MAREKANI NA UINGEREZA ZINAINGIA TANZANIA BILA BREKI?
- KAMUSI YA ISIBATI
-
Links
-
Archives
- May 2006 (2)
- April 2006 (14)
- March 2006 (12)
-
Categories
-
RSS
Entries RSS
Comments RSS
Sikujua kabisa mengi ya misamiati hii ya hisabati. Asante. Tunaelimika.
Nitakupa mawazo yangu ili kuchangia katika ujenzi wa kamusi hiyo.
Ile degree yako ya Kiswahili na Hisabati sasa inajidhihirisha bayana katika hili.Makene alikuwa na hoja siku moja aliponitwangia simu kuwa kuna haja ya blogu hizi kuwa na wataalamu wa fani anuai. Kumbe mpo isipokuwa hamvuni. Vuma mwanangu.
Here are some links that I believe will be interested
ninabashasha rojo rojo jinsi kamusi imenielimisha endelea vivyo hivyo mola awaangazie,ningependa mnitumie msamiati zaidi kwenye e-maile yangu .Asanteni sana
ONLINE – DRUGSTORE!
PRICES of ALL MEDICINES!
FIND THAT NECESSARY…
VIAGRA, CIALIS, PHENTERMINE, SOMA… and other pills!
Welcome please: pills-prices.blogspot.com
NEW INFORMATION ABOUT PAYDAY LOANS!
Welcome please: payday-d-loans.blogspot.com
GOOD LUCK!
Asante kwa kazi yako njema!
Ebu, jaribu kuto maelezo ya maneno mengi yapatikayo ktika isibati!!
Ningependa kuwaomba mnitumie msamiati zaidi kwenye e-mail yangu!Kazi hii ni nzuri!!
kuna marekebisho mengi ya kiswahili hapa. nitaanza na jina la website yako…. kwa kiswahili sanifu, ni HISABATI, sio isabati angalia hapa:
http://kamusi.co.tz/hisabati
ndugu mtunzi,
kweli nimefurahishwa na muamko wako unaolenga kupanua matumizi ya kiswahili katika hisabati na fizikia. Pamoja na pongezi hizo ningekushauri kupekua vitabu mbali mbali vinavyotumika nchini Tanzania katika kueneza elimu ya msingi (Primary School Education). Kuna maneno mengi ya kitaalamu ya kiswahili ambayo yangekusaidia: kwa mfano kanuni (formula),tarakimu (digit),pembe/pembetatu (angle/triangle),mshazali (diagonal), sambamba (parallel),nyuzi (degree), na mengine mengi. Umeanza jambo jema lakini si haba kwangu kunena kuwa “mtaka cha uvunguni sharti ainame” kwani ukita chako “chema” kipate “kuelea” basi huna budi “kiundwe”. Nasema tena hongera kwa mwanzo mzuri