HAMNA UBAKAJI KATIKA NDOA.
Mitindo mibaya ya kimagharibi inanyemelea jamii za Kiafrika kwa kasi
mno. Wanawake hasa walioelimika wameambukizwa ndwele na wanaharakati
wanaodai kwamba wanatetea haki za mwanamke. Nikiegemeza mjadala wangu
katika misingi ya dini ya Kikristo ni kwamba haikuwa mapenzi ya MWENYEZI
MUNGU mwanamke kusema kwamba anadai haki zake. Aidha Biblia takatifu
inasema mwanamke anastahili kuwa mnyenyekevu kwa mumewe. Naye mwanamume
ameshauriwa kumpenda mkewe.
Panapo unyenyekevu na mapenzi basi hamna dhana ya ubakaji. Iwapo bwana
ana nyege mkewe anastahili kuwa tayari kumkidhia haja zake. Panapo
mapenzi basi mume atajua kwamba mkewe si panya kiasi cha kujifungua watoto
kila kukicha. Mapenzi vilevile yatapelekea mume kutambua kwamba mkewe
anaugua hivyo basi itakuwa kumuumiza iwapo atadai ngono.
Dhana hizi za mwanamke aliyeolea kudai kwamba alibakwa na mumewe ni
potovu na zinastahili kupingwa kwa vyovyote vile. Haikosi ndio sababu
wanaharakati hawa wanadai mume na mke ni viumbe sawa. Haiwezekani abadan
katan! Mume aliumbwa kwanza Biblia inasema kisha MUNGU akaona kwamba ipo
haja ya huyu mwanamume kuwa na msaidizi. Hivyo nafasi ya mwanamke
katika jamii inayoongozwa na maadili ya dini ya Kikristo ni ya msaidizi.
Haifai kamwe mwanamke kudai ukurugenzi katika familia.
Ukweli ni kwamba iwapo wanawake wataendelea kubugia sera za magharibi
bila kuzihakiki na kuzipigia maswali basi watajioa wenyewe. Waume zao
watawataliki na walioelimika wataozea nyumbani mwa mama zao.
Watakaobarikiwa ni wale wasio na elimu na wanaotambua uanauke ndio nini.
MISHAHARA YA WABUNGE INAUMIZA WANANCHI.
Bunge litahudhuriwa na wabunge iwapo mjadala utahusu nyongeza ya mishahara yao. Ijapo mijadala ya jinsi ya kupunguzia raia umaskini basi bunge litahudhuriwa na Kilemi Mwiria peke yake. Hawa 'waheshimiwa' wanajua kuzua mijadala kama vile 'Donde bill', 'Keter bill' n.k. lakini hamna yeyote ameshawahi kuzua mjadala wa 'kupunguza mishahara ya wabunge'.
Ni kosa na laana kubwa kuomba misaada kwa madai eti mnataka kupunguzia raia umaskini kisha badala yake mnajilimbikizia misaada hii kama nyongeza ya mishahara. Nchi inayotegemea misaada kama Kenya haifai kuwa inawalipa wabunge nusu milioni na zaidi. Huyu ni mbunge eti, ijapo waziri basi atapokea milioni mwisho wa mwezi. Haikosi ndio sababu madeni ya Kenya ni mengi kupindukia. Marekani yenyewe isiyokuwa na madeni haiwapi wanasiasa wake kiasi kama hiki cha pesa. Uingereza vilevile tumeelezwa kwamba mmoja wa wanasiasa wake huenda kazini kwa baiskeli.
Ijapo kuomba misaada hata akina Professa Kibwana na wenzake huvua uprofesa na kutia saini misaada hii kuja. Akilini mwao huwazia tu namna ambavyo misaada hii itawasaidia kupokea mamilioni ya pesa kila mwisho wa mwezi. Mradi mlipa kodi ambaye ni raia wa kawaida atalipa, mbona professa ajisumbue kuhakiki athari za mikopo kwa raia wa kawaida? Mirundiko ya madeni kama haya ndiyo yamepelekea ushuru kupanda, na serikali kuanza kuwalazimisha wafanyibiashara kutumia mitambo ya kurekodi mauzo yao.
Nikidhani huu unastahili kuwa mkataba kati ya raia na serikali ijayo mwaka wa 2007. Kwamba tutawapa kura tu iwapo watatuahidi kuwa watapunguza mishahara yao. Hivi ndivyo wakenya wanawaambia akina Uhuru, Kalonzo, Kibaki, Raila, Ruto na Balala. Sijajua sababu ya mwalimu kupokea elfu kumi kisha mbunge kupokea milioni kama mshahara. Je ina maana mbunge hula dhahabu huku mwalimu akila sukuma wiki? Je ina maana kinyesi cha mbunge ni tofauti na cha mwalimu? Je ina maana mbunge huishi mwezini huku mwalimu akiishi duniani?
-
Recent
- MAREKANI INAVYOFADHILI VITA BARANI AFRIKA.
- MISHAHARA YA WABUNGE KENYA: WIZI! WIZI! WIZI!
- SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI.
- UBAKAJI: NJOKI NDUNG’U ANAFICHA HABARI FULANI.
- MADHARA YA KUWEPO SARAFU AINA MOJA AFRIKA MASHARIKI.
- KUNA HATARI YA KALONZO MUSYOKA KUWA RAIS?
- NAMNA YA KUPIMA UBORA WA MAISHA.
- KIFO NI NINI?
- KITOTO CHA MAREKANI KINASAFIRI ULIMWENGUNI ZAIDI YA MHADHIRI CHUONI AFRIKA.
- KUTOJUMULISHA MIKOPO YA WAFADHILI: HEKO SERIKALI
- MBONA MAREKANI NA UINGEREZA ZINAINGIA TANZANIA BILA BREKI?
- KAMUSI YA ISIBATI
-
Links
-
Archives
- May 2006 (2)
- April 2006 (14)
- March 2006 (12)
-
Categories
-
RSS
Entries RSS
Comments RSS